Pages

Thursday, January 31, 2013

Breaking News: Sumalee Afiwa Na Baba Yake Mzazi...


 Msanii kutoka hapa nchini, Sumalee au maarufu kama "Mzee wa Hakunaga" amefiwa na baba yake mzazi masaa machache yaliyopita.
      Sumalee ambae ni msanii kutoka Tanzania anaefanya shughuli zake za kimuziki akitamba na ngoma zake kadhaa kali kama "HAKUNAGA" na nyinginezo amekutwa na msiba huu huku yeye akiwa nchini Uingereza katika kazi zake za muziki.
Sumalee pia alimpoteza mama yake mzazi akiwa nchini Marekani kikazi.

50 Cent Azungumzia Shambulizi La Risasi Kwa Rick Ross...

Kama ulisikia, Jumapili hii rapper kutoka Miami, Rick Ross alirushiwa risasi na watu wasiojulikana akiwa na gari yake aina ya Rolls Royce na kunusurika kuuawa... Sasa... Rapper 50 Cent azungumzia tukio hili na kuliita kuwa lilipangwa. "Staged"
     50 Cent ambae amekuwa kwenye beef na Rick Ross kwa muda mrefu sasa, amesema hili limekuwa kama tukio lilipangwa na la kudanganya. Rapper huyo anasema, kama hakukua hata na matundu ya risasi katika gari hiyo aliyokuwa anaendesha jamaa, then huu wote ni uongo.
50 Cent alitweet, "Hahaha fat boy hit the building? lol it looks staged to me. No hole’s in da car".Ripoti ya police wa eneo hilo, Fort Lauderdale pia ilisema, risasi nyingi zilirushwa ila hakuna hata moja iliyolipata gari alilokuwa anaendesha Rick Ross.

Hatimaye KHLOE KARDASHIAN Nae Apata Mimba...

 Mtoto alietoka kwenye familia ya kati ya LAWYERS walioweza kumchomoa mcheza American Footballer O.J SIMPSON kwenye sakata la kesi ya mauaji, huyu si mwingine ni mtoto wa Robert Kardashian bibie Khloe Kardashianambae kwa sasa ni mtangazaji wa kipindi kinachoangaliwa sana nchini Marekani na dunia nzima The X-Factor - US.
         Kutokana na muda mrefu sana kuhangaika kupata mtoto bila mafanikio bibie Khloe Kardashian na mumewe Basketballer LAMAR ODOM inasemekana sasa miracle imetokea na wanatarajia kupata mtoto baada ya kusemekana kuwa TV Star huyo ana UJAUZITO tayari.
         Maneno haya yametoka kwenye Notorious Website MediaTakeOut.com. Wanandoa hawa walikua wazi kabisa kuhusu Maisha yao na tatizo la kupata mtoto la mwanadada huyo kwenye kipindi cha kifamilia ambacho ndio kikubwa kuliko vyote na kina watazamaji wengi sana kuliko reality shows nyingine nchini marekani, Keeping UP with The Kardashians.
         Habari hizi ziletea kuongezeka kwa ujauzito ndani ya familia ya Kardashian and Jenner ambapo KIMKardashian na KANYE WEST nao wakiwa wanategemea mtoto hivi karibuni.

[PHOTOS] Video Making Ya Me N' You Wa Ommy Dimpoz Na Vanessa Mdee...

 Check baadhi ya picha katika utengenezwaji wa video mpya itakayokuja ya Ommy Dimpoz featuring Vanessa Mdee...
Rain Dance?? Oh... Yeah... Ni ME N' YOU , wimbo ambao mimi na wewe hatuwezi bisha kuwa unafanya vizuri sana radioni... na video ndo inatengenezwa... tusubiri tuone kama video ya wimbo huu uliotokea kupendwa sana...

[Video] Alicia Keys Akiimba Obama's on Fire...


Star wa miondoko ya R&B kutoka America, mwanadada Alicia Keys alikuwa ni miongoni mwa wasanii ambao walipata shavu la kutumbuiza kwenye sherehe za kumuapisha Rais Barack Hussein Obama.
       Alicia aliimba wimbo wake wa ''Girl On Fire'' na kuubadilisha kwa kuimba ''Obama's on Fire'' jambo ambalo liliwafurahisha watu wengi ambao walihudhuria sherehe hizo.

[Picha] Beyonce Amnunulia Mama Yake Jumba La Kifahari Linalogharimu $5.9 Million...


Star kutoka Hollywood Beyonce, amemnunulia mama yake mzazi Tina Knowles jumba la kifahari ambalo limemgharimu kiasi cha zaidi ya dolla za kimarekani $5.8 Million. Jumba hilo ambalo lipo katika mji wa Houston ni kubwa sana na lina vitu vingi ambavyo hata huwezi kufikiria kama huyo mama atakuwa kama anavitumia. 
Check picha zaidi za jumba lenyewe hapa chini....

Shakira Ajifungua Mtoto Wa Kiume...

 Nyota wa pop kutokea nchini Colombia, Shikara hatimaye jana amejifungua mtoto wa kiume mjini Barcelona.Shakira ametoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa wanafuraha sana yeye na mumewe kwa kufanikiwa kupata mtoto wa kiume mbae wamempa jina la Milan Pique Mebarak.
Hongera sana mwanadada Shakira kwa kupata mtoto...

[Video] Kilivyonuka Kwenye Uzinduzi Wa Track Mpya Ya Izzo Bizness - BALL PLAYER

  Video hii inawaonesha wasanii, Izzo Bizness, Quick Rocka na Mangwea wakiwa katika Studio za Clouds FM katika kipindi Cha XXL cha mchana wakati wakitambulisha track mpya ya Izzo Bizness inayofahamika kama BALL PLAYER...
     Jamaa walifanya vyema sana kwenye interview hiyo na B Dozen, Ma-champaign, freestyles na fun nyingine zilizo-happen....
Icheck mwenyewe hapa chini...http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=YqXxfggzSI4

[AUDIO] Brand New: Diva ft. Mr. Blue - Mgonjwa Kwa Raha Zako

 Its A Brand New Track kutoka kwa Diva, Loveness Love ikifahamika kama MGONJWA KWA RAHA ZAKOakimshirikisha Byser a.k.a Mr. Blue...The track imerekodiwa na producer Mona Gangster...
Isikilize hapa chini:http://www.hulkshare.com/

Timbaland Apoteza Saa Yenye Thamani Ya $1.8 Million...


 Music Producer mkongwe kutokea nchini Marekani maarufu kama Timbaland ambae pia ni mwanamuziki maarufu sana amepoteza saa yake ya gharama kubwa.
       Timbaland ambae alishafanya kazi na Aaliyah, Justin Timberlake, Nelly Furtado, Kelly Hilson na wengine wengi na track zao kufanya vizuri na kumjazia umaarufu zaidi ni kuwa ameamua kuishtaki kampuni ya insurance ya''American Home Insurance'' , baada ya kuchelewesha madai yake baada ya kupotelewa na saa yake yenye thamani ya dolla za kimarekani $1.8 Million. 
        Timbaland amedai kuwa saa yake ilipotezwa na mtoto wake wa k*** mwenye miaka miwili, ambaye aliichukua na kuichezea na baada ya hapo kuitupa pasipojulikana. Timbaland ameamua kuishtaki na kuidai $1.8 million na gharama zote za kesi kampuni hiyo.