Pages

Friday, June 28, 2013

VIDEO YA WEMA SEPETU AKIWAPOROMOSHEA MATUSI MAZITO WAFANYAKAZI WAKE WA NDANI


STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi.  

Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.  

Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua tatizo. 

Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.

Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.

Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.  

Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na kuanza kutoa mkong’oto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele yake.

  Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni isiyoandikika  kutokana na ukali wake.