Pages

Sunday, May 5, 2013

BAADHI YA WASHUKIWA WA UJAMBAZI NYUMBANI KWA FINA MANGO WAKAMATWA



Fina Mambo akiwa na familia yake

Kupitia Twitter ameeleza:
Lile kundi la majambazi lilokua likifanya uvamizi wa nyumba zipatazo 7 (kwangu ilikua ya 4) maeneo ya Kawe hadi Mbezi, ilisemekana ni kundi la watu 40 waliosambaa kuanzia Kawe (makao makuu) Mikocheni, Kinondoni mpaka Mbagala, Wameanza kukamatwa.


Polisi Kawe inashikilia watu 7 ambao walikutwa na baadhi ya vitu pamoja na bastola 1 na Gobole 1 matching risasi zilizokutwa maeneo ya tukio.


Waliokamatwa wanaongea na kusema kote walikopeleka mali kuviuza. Ni juhudi za kusifiwa za mmoja wa wahanga maana aliamua kulifatilia swala.


Hili mpaka mwisho wake baada ya kuvamiwa na risasi kupigwa ndani kwake. Kwa ushirikiano na wasamaria wema waliotoa info pamoja na Kawe Police wamekamatwa. Kidogo twaweza lala kwa Amani sasa.


Fina Mambo alivamiwa na majambazi wafikao wanane nyumbani kwake na kupora mali na fedha.
Screenshot 2013-03-25 at 06.49.53
Screenshot 2013-03-25 at 06.50.00