Pages

Thursday, January 31, 2013

Timbaland Apoteza Saa Yenye Thamani Ya $1.8 Million...


 Music Producer mkongwe kutokea nchini Marekani maarufu kama Timbaland ambae pia ni mwanamuziki maarufu sana amepoteza saa yake ya gharama kubwa.
       Timbaland ambae alishafanya kazi na Aaliyah, Justin Timberlake, Nelly Furtado, Kelly Hilson na wengine wengi na track zao kufanya vizuri na kumjazia umaarufu zaidi ni kuwa ameamua kuishtaki kampuni ya insurance ya''American Home Insurance'' , baada ya kuchelewesha madai yake baada ya kupotelewa na saa yake yenye thamani ya dolla za kimarekani $1.8 Million. 
        Timbaland amedai kuwa saa yake ilipotezwa na mtoto wake wa k*** mwenye miaka miwili, ambaye aliichukua na kuichezea na baada ya hapo kuitupa pasipojulikana. Timbaland ameamua kuishtaki na kuidai $1.8 million na gharama zote za kesi kampuni hiyo.