Pages

Thursday, May 30, 2013

"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK


Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.

Sunday, May 5, 2013

NEW MUSIC : PHD ft. Mr. Blue - REST OF MY LIFE ...

PHD ameachia ngoma nyingine ... Hemedy ambae mara ya mwisho he dropped GOING CRAZY iliyofanywa na producer PANCHO LATINO kutoka B'HITZ MUSIC GROUP ...
Hemedy ametupa jiwe jingine ... REST OF MY LIFE ambalo in here amemshirikisha "swagg boy" Mr. Blue ...
Sikiliza na unaweza download REST OF MY LIFE hapa chini :

BRAND NEW MUSIC & LYRICS : AY ft. Fid Q - JIPE SHAVU ... Prod. By Q The Don ...


Ni ngoma mpya kutoka kwa mwanamuziki AY ambae anazidi kufanya vizuri katika muziki ... Hapa ame-drop JIPE SHAVU ...
Katika ngoma hii, AY amemshirikisha rapper kutoka Mwanza maarufu kama FID Q, ikiwa imetengenezwa katika studio za MPO AFRICA huku mdundo ukiwa umesukwa na producer Q Tha Don ...
Kuwa wa kwanza kusikiliza na download JIPE SHAVU hapa chini :
Hapa chini ni mashairi/lyrics za ngoma hii mpya ya AY ... #JipeShavu ...
Verse 1:

Nachana style zaidi ya kumi bado kiwango same/
Kwenye speaker unamsikia mastermind wa hii game/
Toka BC game,mpaka AC game/
Wanajaribu hata kugeza hawana Edu-Tain/
Nasmile,wanavyoscream M BACK AGAIN/
Chillax,usipanic kwani where have you been/
Bila msoto maisha haya mjomba huwezi gain/
Kanyaga moto acha utoto then life maintain/
Napata moyo navyosikika toka Jozi mpaka Lagos/
Bado mnakuna vichwa level hizi chafu mikosi/
Nimetoka mbali na hii game bado naidai/
Ndio maana sivimbi kichwa na Ufame till I die/
Usiwe bingwa wa kuhonga na home wanalala njaa/
Nyumbani umeacha mboga moja ka komba ulala baa/
Ujanja kuweka heshima nyumbani na is kuweka baa/
Unashangaa?? Stuka huu sio muda wa kuzubaa

Chorus:
Fid Q:

Jipe shavu,kama unajipa una hizi sifa na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa,
Una Cash?Money,we ni Hustler?flani
Unasupport yako familia na uko real x2
AY:

Jipe shavu,kama unajipa una hizi sifa na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa,
Una Chase?Money,we ni Hustler?flani
Unasupport yako familia na uko real x2

VERSE 2:

(Fid Q)
Jipe shavu.. kabla haujajipa uwe na hizi na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa..
una cash- money.. wewe ni hustler.. fulani../
Ulikuja na DASH kama DAMON ukazi-Chase kama DAMIAN/
jipe shavu ukiwa na ubavu wa u - billionea/
Haters watashow LOVE kwa HI 5 everywhere/
'' C E O wa CHEUSIDAWA TV'' yeah.. iliyoanza kwa flipcam/
ukinikuta club utapagawa.. njoo u-Sip some/
Flow hizi tamu/ zinaleta SNOWS ndani ya DAR ES SALAAM/
na mie ndo BOSS bado haujanifahamu?/
TROUBLESOME..na hizi lyrics sio bubble gum/ Multi- Syllabic acheni ubishi hii sio double rhyme..

Chorus:
Fid Q:
Jipe shavu,kama unajipa una hizi sifa na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa,
Una Cash?Money,we ni Hustler?flani
Unasupport yako familia na uko real x2
 AY:
Jipe shavu,kama unajipa una hizi sifa na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa,
Una Chase?Money,we ni Hustler?flani
Unasupport yako familia na uko real x2


Verse 3:
Beware,usinifuate shika nukuu,fanya mbwembwe huko uliko ila usije njia kuu,
Mdundo mzito wa Q
Michano ya level ya juu
Kazi inaisha kabla ya kuanza mbele ya me and Fid Q,
Ukitaka kunijua jiandae kujilaumu
Bora uhairishe zoezi kubakie tu kunifahamu
Jipe shavu ulikuja mjini mnyonge mzeiya sasa una mabavu,unasurvive,na wengine unawapa shavu
Jina lavuma Afrika nzima nazidi tu kujituma
Nyuma na support nzima Mtwara to Musoma
Dar to Kigoma ,A Town,Moro to Ruvuma
Tanzania nzima so unatamani hata kugoma
Umenisoma?mchaka wa soka ka mchizi Chonka
Chini kwa chini ka Inju bin Unuki mi nasonga
Mkononi Michael Kors na 3 smart phones
Border nazidi cross huniambii we bitozi
Simu nyingi zinazotoka na kuingia ni za biashara
We bwabwaja,scratch yo balls mzembe zidi lala
Ujanja kupeleka faida bank ya ile uliyoinvest
Bora uhairishe kabla hujaniface

Chorus:
Fid Q:
Jipe shavu,kama unajipa una hizi sifa na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa,
Una Cash?Money,we ni Hustler?flani
Unasupport yako familia na uko real x2
AY:
Jipe shavu,kama unajipa una hizi sifa na kama una hizi sifa hakikisha watu walikupa,
Una Chase?Money,we ni Hustler?flani
Unasupport yako familia na uko real x2

Credits:
AY Featuring Fid Q
Jipe Shavu
Produced by Q the Don
Mpo Afrika Studio

MOUNTAIN DEW Yakatisha DEAL Yake Na LIL WAYNE ...


Rick Ross amekuwa sio wa kwanza baada ya deal yake na REEBOK kukatishwa baada ya kuandika mashairi yake yanayochochea vitendo vya ubakaji ... LIL WAYNE amefuatia ... hii ni baada ya MOUNTAIN DEW kumuadhibu kwa kukatisha deal yao baada ya mistari yake iliyomgusa mwanaharakati wa haki za kiraia Emmett Till.
“Beat that pu**y up like Emmitt Till,” ame-rap LIL WAYNE, rapper kutoka New Orleans katika original remix ya ngoma ya Future inayojulikana kama “Karate Chop.”
According to LIL WAYNE, mistari hiyo ilifutwa baadae na yeye kutuma barua kwa familia ya mwanaharakati huyo na kuomba msamaha lakini hii haikutosha ...
Emmitt Louis Till alikuwa ni mvulana mwenye asili ya kaifrika nchini Marekani ambaye aliuawa huko Mississippi akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kubainika kuwa na mwanamke mweupe ...
Pamoja na kuyatoa, familia ya TILL imekuja juu na kumshutumu LIL WAYNE kwa matumizi ya jina hilo la ndugu yao ...
Viongozi wa Mountain Dew walichukua maamuzi siku ya Ijumaa na kutangaza kukatisha mkataba huo na LIL WAYNEmwenye miaka 30 sasa ...
Ndugu wa Emmitt Louis Till wameomba mkutano na rapper huyo baada ya barua iliyotumwa na Lil Wayne ili kuweza ku-discuss makubaliano kati ya rapper huyo na uongozi wa PepsiCo ...

Baada Ya SHOSTEEZ ... LAMAR Asaka Kundi La Kiume ..


Producer mkali kutoka FISH CRAB COOKOUTS maeneo ya KARIAKOO anasaka kundi la vijana wa kiume ... LAMARambae ndiye mmiliki wa studio hiyo ameshaunda kundi la wasichana linalofahamika kama SHOSTEEZ na sasa anataka la wavulana ...
LAMAR amekuwa na programme hiyo toka mwaka jana na sasa ametangaza hivyo kupitia kurasa zake tofauti za mitandao ya kijamii akisaka vipaji hivyo kwa ajili ya kuviendeleza ...
Check alichoandika hapa chini kupitia kura yake ya TWITTER ...

KIINGEREZA CHAMUUMBUA DIAMOND...MASHABIKI WAMPA MAKAVU




Katika pitapita  instagram kuna picha ya msanii Diamond Platnumz alipost (hiyo hapo juu), na hapo wakatokea watu kukosoa kingereza alichotumia huku wengine wakionekana kutetea. JAMANI ENGLISH si Lugha yetu jamani. angalia hapa chini


BAADHI YA WASHUKIWA WA UJAMBAZI NYUMBANI KWA FINA MANGO WAKAMATWA



Fina Mambo akiwa na familia yake

Kupitia Twitter ameeleza:
Lile kundi la majambazi lilokua likifanya uvamizi wa nyumba zipatazo 7 (kwangu ilikua ya 4) maeneo ya Kawe hadi Mbezi, ilisemekana ni kundi la watu 40 waliosambaa kuanzia Kawe (makao makuu) Mikocheni, Kinondoni mpaka Mbagala, Wameanza kukamatwa.


Polisi Kawe inashikilia watu 7 ambao walikutwa na baadhi ya vitu pamoja na bastola 1 na Gobole 1 matching risasi zilizokutwa maeneo ya tukio.


Waliokamatwa wanaongea na kusema kote walikopeleka mali kuviuza. Ni juhudi za kusifiwa za mmoja wa wahanga maana aliamua kulifatilia swala.


Hili mpaka mwisho wake baada ya kuvamiwa na risasi kupigwa ndani kwake. Kwa ushirikiano na wasamaria wema waliotoa info pamoja na Kawe Police wamekamatwa. Kidogo twaweza lala kwa Amani sasa.


Fina Mambo alivamiwa na majambazi wafikao wanane nyumbani kwake na kupora mali na fedha.
Screenshot 2013-03-25 at 06.49.53
Screenshot 2013-03-25 at 06.50.00

"BILA CONDOM HUWEZI KULIFAIDI PENZI LANGU HATA UKINIHONGA MABILIONI"...SHILOLE


Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa  jina  la   shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila  condom )  ....

Akiongea kwa  kujiamini ,Shilole  alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama  hana  kondom  mkononi.....

Msanii  huyo  alienda  mbali  zaidi  na  kuzilaani   kauli   za  baadhi  ya  watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM"  ladha ya mapenzi inapungua.Yeye  anadai  kuwa  ni  mdau  wa  "GEMU"  hilo  na  huwa  anatumia  NDOM  kama  kawa  na  hufurahia  kama  kawaida...

" Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimezea  mate....Waje  tu , lakini  bila  KINGA wataambulia  PATUPU!!” Alisisitiza Shilole

PICHA ZA JENGO LINALOFANANA NA UUME ZATOLEWA NA GAZETI LA CHAMA TAWALA NCHINI CHINA...



Gazeti la chama tawala cha china, People’s Daily ambalo limezoea kuwa kitovu cha kusambasa habari, sasa limejikuta likiwa habari baada ya watu wenye fikra za kitukutu kuona jengo jipya la gazeti hilo limefanana na nyeti za kiume.
 
Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida, picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama “Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.

Watu wengi wameeleza kuwa kwa kutumia ubunifu kidogo tu wa photoshopping, unaweza kuambatanisha picha ya jengo hilo, ambalo raia wamelipa nickname “Giant Pen*s” au “Uume mkubwa,”katikati ya “miguu” ya jengo lingine maarufu nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV cha China Central Television (CCTV,) linalojulikana kwa nickname ya “Big Und*rpants”building au Jengo la Chupi Kubwa.

 Habari za utani huo zilifikia wakubwa nchini humo ambao walikerwa na kuamua kuwaharibia watu raha zao kwa kuamuru website ya Sino Weibo ku-block search zote zinazotafuta picha au habari za jengo hilo. 


Kwa sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe“kuendana na sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi kuonyeshwa."
 
Mwandishi wa Reuters, Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations miongoni mwa vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”