Rapper Nikki Mbishi leo anasheherekea siku ya kuzaliwa kwake. Jina kamili anaitwa NICAS JOHN MARWA MACHUCHE alizaliwa mwaka 1989 mwezi na tarehe kama ya leo.
Mbishi alimaliza elimu yake ya msingi mwaka 2003 katika shule ya msingi Juhudi na kujiunga na elimu yake ya sekondari katika shule ya Juhudi Secondary 2004 - 2007, baada ya hapo alisoma chuo cha Mbeya Institute Of Science And Technology.
Baada ya hapo, Nikki alijitosa kwenye fani ya muziki ambapo hadi sasa Nikki bado anafanya akiwa na mtoto mmoja ambae anaitwa Malcom Zohan. Hadi sasa Nikki Mbishi bado hajaoa na anajishughulisha na kazi yake ya kuchana ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa midundo ya kazi za wasanii tofauti.
Pia rapper huyu anasheherekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na Marehemu Miriam Makeba "Mama Africa" ambapo kama angekuwa hai hadi sasa basi angetimiza umri wa Miaka 81. Miriam Makeba aliwahi kushinda tuzo za Grammymwaka 1966 kama Best Folk Recording kutoka South Africa akiwa ni msanii wa kwanza kutoka Africa kushinda tuzo hiyo.
Kampuni ya Google inamuenzi mwanamama huyo katika siku yake hii kwa kuweka mchoro wa picha yake katikaHomepage ya Google.
_______________________________