Kamati iliyoundwa kuchunguza vitendo vya udhalilishaji na kuporwa vitu vyao wanavyofanyiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wanaoishi katika hosteli zilizopo Kigamboni Manispaa ya Temeke imebaini hakuna wanafunzi waliofanyiwa vitendo hivyo.
Kamati hiyo iliyoundwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Polisi jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova baada ya kuwahutubia wanafunzi hao katika Viwanja vya Machava, ilijumuisha wanafunzi wanne wa IFM na wakuu wa upelelezi kutoka kanda hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Englebert Kiondo, alisema kamati hiyo ilichunguza kwa kina madai hayo ya wanafunzi, lakini hakuna na hata moja walilobaini kuwa na ukweli .
Alisema suala la ulawiti walilodai wanafunzi, walijaribu kufuatilia kwa ukaribu kutumia dawati la jinsia ikiwamo kuwauliza wanafunzi hao ni nani alifanyiwa kitendo hicho, lakini hamna hata mmoja aliyejitokeza kusema amefanyiwa.

“Tuliwauliza wanafunzi ni nani amefanyiwa kitendo kama hiki ili tujue cha kufanya, lakini hakuna aliyejitokeza kukiri kuwa alilawitiwa tofauti na walivyodai hivyo wakati wa maandamano ,” alisema Kamanda Kiondo.