Pages

Tuesday, March 5, 2013

"NATUMAINI KWAMBA NITASHINDA UCHAGUZI UJAO"...ROBERT MUGABE


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema kwamba ana matumaini ya kushinda katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo.

Akizungumza hapo jana mjini Harare katika sherehe yake ya kuadhimisha kuzaliwa kwake ambapo amefikisha miaka 89 Mugabe amesema, anaamini atamshinda hasimu wake katika uchaguzi ujao wa rais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu na kubakia  madarakani kwa miaka mingine mitano.

Aidha rais huyo mkongwe wa Zimbabwe amewatuhumu wapinzani wake kuwa, wanakusudia kuzusha machafuko ya kisiasa nchini humo kwa lengo la kumfanya ashindwe kwenye uchaguzi ujao.

Hivi karibuni Mugabe alitangaza kushiriki kwa mara ya sita katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambayo ameiongoza kwa zaidi ya miaka 33.

via Radio Teheran