Pages

Thursday, January 31, 2013

50 Cent Azungumzia Shambulizi La Risasi Kwa Rick Ross...

Kama ulisikia, Jumapili hii rapper kutoka Miami, Rick Ross alirushiwa risasi na watu wasiojulikana akiwa na gari yake aina ya Rolls Royce na kunusurika kuuawa... Sasa... Rapper 50 Cent azungumzia tukio hili na kuliita kuwa lilipangwa. "Staged"
     50 Cent ambae amekuwa kwenye beef na Rick Ross kwa muda mrefu sasa, amesema hili limekuwa kama tukio lilipangwa na la kudanganya. Rapper huyo anasema, kama hakukua hata na matundu ya risasi katika gari hiyo aliyokuwa anaendesha jamaa, then huu wote ni uongo.
50 Cent alitweet, "Hahaha fat boy hit the building? lol it looks staged to me. No hole’s in da car".Ripoti ya police wa eneo hilo, Fort Lauderdale pia ilisema, risasi nyingi zilirushwa ila hakuna hata moja iliyolipata gari alilokuwa anaendesha Rick Ross.