Pages

Friday, February 1, 2013

[PHOTO] Check Artwork Ya Album Mpya Ya Lil Wayne...

Rapper kutokea kundi la Cash Money [YMCMB] maarufu kama Lil Wayne ameachia Art Work ya Cover ya album yake mpya inayoitwa ''I Am Not A Human Being II''.
Kazi hiyo ya ubunifu na utengenezaji mzima wa hiyo cover art imefanywa na kampuni anayoimiliki rapper Kanye Westambayo inaitwa Creative Content Company.
Lil Wayne anatarajia kuachia album yake hiyo ifikapo mwezi March mwaka huu.

Drake Kuachia Track Mpya Kwenye Tuzo Zijazo Za Grammy…

Msanii kutokea America ambae ni mzaliwa wa Canada akiwa chini ya label ya Young Money [YMCMB] maarufu kwa jina la Drizzy Drake hivi karibuni ataachia ngoma yake nyingine.
Drake ambae aafanya vyema na ngoma zake kama Take Care, The Motto, No Lie akiwa amempa shavu rapper 2 Chainz na ngoma hiyo kufanya vizuri katika media mbali mbali anatarajia kuachia ngoma yake hiyo mpya siku ya Tuzo Za Grammy ambayo imesikika kuwa ameipa jina la "Started From The Bottom’’.Track hiyo ambayo imetengezwa na Producer ambae pia ni rafiki yake wa karibu Noah "40" Shebib.
Drake pia amekuwa nominated kwenye tuzo hizo ambazo hadi sasa zinatimiza Miaka 55 tangu kuanzishwa kwake.

[AUDIO] Brand New: Kitale ft. Sharo Millionea - Midezo Hili Toto...

Hii ni track mpya kutoka kwa msanii Kitale ambayo amemshirikisha marehemu Sharo Milionea wakati wa uhai wake, ngoma inaitwa ''Midezo Hili Toto''.
Kitale pia ni msanii wa maigizo akiwa upande wa uchekeshaji zaidi akijipatia umaarufu kupitia sauti na muonekano wake wa kiteja...http://hu.lk/19uzg90vqw08

[PHOTOS] Je Ni Kweli Lil Wayne Amekata Rasta Zake??!!...


Rapper kutokea kundi la Young Money Cash MoneyLil Wayne amesadikika kubadili muonekano wake hasa kwenyeRasta zake. Rapper huyo ambaye alianza kufuga Rasta zake kuanzia miaka ya 2000 akiwa na kundi la Hot Boyzalionekana sehemu jana akiwa na Rapper Big Boi [Outkast] akionekana kutokuwa na Rasta zake zilizomuweka Lil Wayne katika muonekano mpya kabisa.Lakini ukweli kuhusu picha hizi ni kuwa Lil Wayne hajakata Rasta zake ila ni muonekano ambao umewachanganya fans wake katika picha hizi. Lil Wayne bado ana Rasta zake kama kawa isipokuwa katika picha hizi zilionekana kufungwa kwa nyuma na kusababisha kutoonekana.

Sony Watoa Simu Inayoweza Kutumika Ndani Ya Maji...

Kampuni ya Sony jana imetoa toleo jingine la simu ambalo ni Sony Xperia Z ambapo simu hiyo imetengenezwa katika mfumo wa kutokuruhusu maji yaweze kuidhuru simu hiyo kwa muda wa nusu saa hivyo unaweza ukapiga picha ukiwa ndani ya maji na hata kuoga nayo na wala isilete matatizo yoyote.
         Simu hiyo pia ina ubora mkubwa wa picha ambao ni High Definition, nyembamba sana yenye urefu wa inchi 13 pia inatumia mtandao aina ya 4G.Pia imenakiliwa kuwa ndio simu ya kwanza duniani kote ambayo imetengezwa katika mfumo wa kuzuia maji [Water Proof]. Msemaji wa kampuni hiyo aliongeza kwa kusema kuwa Unaweza kupiga na kupokea simu ukiwa ndani ya maji ila hajui wewe utaongeaje na utasikiaje ukiwa ndani ya maji. Simu hiyo inategemewa kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu na kuuzwa Pound 450.

Kanye West Na Kim Kardashian Wajenga Jumba La Kifahari Lenye Thamani Ya $ 11 Milioni

 Kama tunavyojua kuwa wawili hawa wakiwa ni wazazi watarajiwa wameonekana wakiwa na malengo makubwa kuhusiana na mtoto wao mtarajiwa. Sasa habari kamili kutoka kwa wapenzi hawa, yaani Kim Kardashian na mwenzieKanye West ni kuwa wametumia zaidi ya Dola Milioni 11 kwa kujenga nyumba yao ambayo wanatarajia kuhamia pindiKim atakapo jifungua.Jumba hilo ambalo limejengwa kwa staili ya Italian Villa maeneo ya Bel Air, California ambapo ndani litakuwa na chumba cha kufanyia mazoezi [Gym], chumba cha kuangalia sinema, Saloon, uwanja wa mpira wa kikapu [BasketBall] pia kutakuwa na bwawa la kuogelea la ndani na nje pia.

[Picha] Wasanii Kutoka USA Waliowahi Kutokea Kwenye Majarida Tofauti Wakiwa Nusu Uchi...

 Hawa ni baadhi ya wasanii wakubwa duniani waliowahi kutokea kwenye kurasa za mbele za majarida makubwa tofauti ya nchini Marekani. Rihanna ambae pia alitokea hivi karibuni katika Jarida la GQ akiwa nusu uchi December mwaka jana.
     Picha hizi ambazo zimekuwa zikitokea katika ukurasa wa mbele kabisa wa majarida haya makubwa na maarufu duniani, zimekuwa zikileta gumzo kwa wafuatiliaji wazuri wa sanaa duniani kote, wengine wakipinga picha hizi na kuziita ni kinyume na maadili na wengine waki-support kwa kuziona zinakwenda na wakati.