Pages

Friday, February 1, 2013

Sony Watoa Simu Inayoweza Kutumika Ndani Ya Maji...

Kampuni ya Sony jana imetoa toleo jingine la simu ambalo ni Sony Xperia Z ambapo simu hiyo imetengenezwa katika mfumo wa kutokuruhusu maji yaweze kuidhuru simu hiyo kwa muda wa nusu saa hivyo unaweza ukapiga picha ukiwa ndani ya maji na hata kuoga nayo na wala isilete matatizo yoyote.
         Simu hiyo pia ina ubora mkubwa wa picha ambao ni High Definition, nyembamba sana yenye urefu wa inchi 13 pia inatumia mtandao aina ya 4G.Pia imenakiliwa kuwa ndio simu ya kwanza duniani kote ambayo imetengezwa katika mfumo wa kuzuia maji [Water Proof]. Msemaji wa kampuni hiyo aliongeza kwa kusema kuwa Unaweza kupiga na kupokea simu ukiwa ndani ya maji ila hajui wewe utaongeaje na utasikiaje ukiwa ndani ya maji. Simu hiyo inategemewa kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu na kuuzwa Pound 450.