Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kupiga show, mwanamuziki Q Chillah alipiga bonge la show katika ukumbi wa disco wa New Maisha Club jana.
Q hakuwa mwenyewe kwani alisindikizwa na wasanii wengi kama H-Baba, Banza Stone, Ally Nipishe, Canal Top, Beka kutoka THT pamoja na Cassim Mganga.
Pia moja ya matukio yaliyosisimua watu wengi katika show hiyo ni pale Q Chillah alipopanda jukwaani pamoja na baba yake ambae zamani alikuwa ni mchezaji mpira, Mzee Shaban Katwila.
Check baadhi ya picha za kwenye show hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo...



