Pages

Thursday, February 28, 2013

Mtandao Wa Google Waja Na "GOOGLE GLASS"... Hii Kali Ya Mwaka...

Tukiongelea neno GOOGLE basi natumaini kila mtu atakuwa anaelewa hasa kwa wale watumiaji wakubwa na wa mara kwa mara wa Internet.
Sasa mpya kutoka kwenye kampuni hiyo ya Google ni kuwa imetoa bidhaa mpya ambayo ipo katika mtindo wa Miwani (Google Glass) yenye uwezo wa kurekodi video na kupiga picha mahali popote utakapo kuwepo.
Google ndio kampuni ya kwanza kuja na Teknolojia hiyo ambayo ni rahisi sana kuitumia.
Imetengenezwa katika mtindo wa kuiamrisha (Command), unachotakiwa kufanya ni kusema ''Ok Glass Take A Picture'' nayo itafanya hivyo na pia itakupa uwezo wa ku-share picha hiyo kwa marafiki, ndugu, washkaji zako papo hapo.
Pia unaweza kuitumia miwani hiyo kwa Video Chat kama ilivyo Skype, pia unaweza kutafuta habari kupitia google, kutasfsiri lugha na mengineyo.
Unaweza kufanya yote hayo bila kutumia mikono yako, kwa nchini Tanzania kifaa hiki kinakadiriwa kuuzwa kwa bei ya Shilingi Millioni 2.2 ambazo ni sawa na dola $1500 za kimarekani.