skip to main |
skip to sidebar
Timbulo Ashukiwa Kukamatwa Na Madawa Ya Kulevya...
Msanii wa kizazi kipya maarufu kama Timbulo ambae anatamba na baadhi ya ngoma zake kama Domo Langu, WaleoWakesho, Samson Na Delila na ngoma hizo kumfanya atambulike zaidi katika tasnia hii ya muziki inasemekana amekamatwa na madawa ya kulevya.Kuna tetesi kuwa msanii amekamatwa mjini Bujumbura, Burundi kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya.Timbulo alikuwa nchini humo akiwa anafanya shows mbalimbali. Bado tunaendelea na kufuatilia taarifa kamili juu ya habari hii.