DHAMIRA ya watu wengi ni kutunza mimba hadi kufikia hatua ya kujifungua lakini wakati mwingine ujauzito unaweza kuchoropoka kutokana na sababu tofauti, iwe kwa kukusudia au bahati mbaya.
Kwenye maisha ya mastaa wetu wa Bongo, wapo waliowahi kupata mimba lakini kutokana na sababu tofauti, zilichoropoka.
Amani linakumegea baadhi ya mastaa hao ambao wengine walianika sababu za mimba hizo kuchoropoka huku wengine wakifanya siri:
AUNT EZEKIEL
Februari, 2011 aliripotiwa kuwa na ujuzito wa mwanaume ambaye mwenyewe hakumtaja lakini haikupita muda mrefu, mimba hiyo ilichoropoka pasipo kuweka wazi sababu.
JINI KABULA
Mwaka jana alijinadi kuwa na ujauzito wa Mbongo Fleva, Maximiliam Bushoke. Mimba hiyo ikadumu kwa miezi kadhaa, ghafla ikachoropoka yenyewe kwa bahati mbaya.
WEMA SEPETU
Kwa upande wake alitundikwa kibendi na aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ lakini miezi kadhaa mbele ikatoka yenyewe kutokana na sababu za kitaalam.
LULU
Mwaka jana aliripoti kwenye vyombo vya habari kuwa na mimba ya muigizaji mwenzake, marehemu Steven Kanumba. Wakati mapaparazi wakiendelea kufanya uchunguzi, ghafla ikadaiwa ‘kuyeyuka’ pasipo kujulikana chanzo.
LADY JAYDEE
Huyu ni mke halali wa Mtangazaji, Gardner Habash. Mwaka 2011 mitandao ya kijamii iliripoti kuwa ni mjamzito na kudaiwa kuwa habari hiyo ilimpa faraja mumewe lakini furaha hiyo iliyeyuka ghafla wakati Lady Jaydee akionekana na tumbo kubwa, ikadaiwa mimba imechoropoka bila sababu kutajwa.
BABY MADAHA
Mwaka 2010 mkali huyo wa filamu na muziki Bongo, alidaiwa kuwa na mimba ingawa mwenyewe hakutaka kuweka wazi lakini baadaye ilidaiwa kuwa alikwenda kuichoropoa nchini Kenya.
JACK WA CHUZ
Mapema mwaka huu aliripotiwa kuwa ni mjamzito lakini mwenyewe hakupenda kuweka mambo yake hadharani. Hata hivyo, vyanzo makini vilidai kuwa mimba hiyo ilikuwa ya mfanyabiashara mmoja jijini Dar lakini baadaye aliichoropoa pasipo kufahamika sababu.
Kesi ya Zumaridi yapangiwa hakimu mpya
-
Hakimu Monica Ndyekobora ameondolewa kusikiliza shauri la jinai namba
12/2022 linalomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wenzake
83 bad...
2 years ago