Pages

Wednesday, February 27, 2013

MAGAZETI YA AFRKA YAPOTOSHWA KUHUSU HABARI ZA MIKE TYSON KUBADILISHWA KUWA MWANAMKE


Tarehe 12/12/2012   iligeuka kuwa siku ya wajinga duniani badala ya April Mosi baada ya magazeti mengi ya Afrika na hasa Tanzania kuingizwa mkenge na habari ya kubuni ya Mike Tyson kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke. 

Bahati mbaya sana ni kuwa bado watanzania wengi yakiwemo magazeti na hata baadhi ya vituo vya radio vimeendelea kuisema habari hiyo ya kupotosha kama vile ni ya kweli.


Habari hiyo hata hivyo iliandikwa mwishoni mwa mwezi November na website ya nchini Uingereza ambayo huandika habari za kubuni iitwayo NewsBiscuit.

Magazeti maarufu nchini yakiwemo Mwananchi na Jambo Leo yaliiandika habari hiyo pamoja na magazeti mengine makubwa barani Afrika kama The Standard la Zimbabwe na website ya Ghana SpyGhana.

Kwa mujibu wa BBC,NewsBiscuit ilidaiwa kuelemewa zaidi jana kutokana na wasomaji kuwa wengi kutoka Afrika.

“Tumepata wasomaji zaidi ya nusu kutoka Afrika katika siku chache zilizopita ambao tungetegemea kuwapata kwa mwezi mzima,” mwandishi wa mtandao huo John O’Farrell aliiambia BBC.

Alisema habari hiyo ilisomwa zaidi ya mara 50,000 katika siku chache tu ikiwa ni mara 20 zaidi ya kawaida.