skip to main |
skip to sidebar
Kanye West Na Kim Kardashian Wajenga Jumba La Kifahari Lenye Thamani Ya $ 11 Milioni
Kama tunavyojua kuwa wawili hawa wakiwa ni wazazi watarajiwa wameonekana wakiwa na malengo makubwa kuhusiana na mtoto wao mtarajiwa. Sasa habari kamili kutoka kwa wapenzi hawa, yaani Kim Kardashian na mwenzieKanye West ni kuwa wametumia zaidi ya Dola Milioni 11 kwa kujenga nyumba yao ambayo wanatarajia kuhamia pindiKim atakapo jifungua.Jumba hilo ambalo limejengwa kwa staili ya Italian Villa maeneo ya Bel Air, California ambapo ndani litakuwa na chumba cha kufanyia mazoezi [Gym], chumba cha kuangalia sinema, Saloon, uwanja wa mpira wa kikapu [BasketBall] pia kutakuwa na bwawa la kuogelea la ndani na nje pia.