Pages

Friday, June 7, 2013

WASHINDI WA TWEET ILIYOMKUNA REGINALD MENGI AKABIDHIWA KITITA CHA SH. MILIONI MOJA

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja mshindi wa kwanza wa shindano la,  "Tweet Wazo Jipya Kuondoa Umaskini", Jilly Gaudence Kyomo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dkt. Donath Olomi. 
Kulia ni mshindi wa pili, Peter George aliyejinyakulia shilingi laki tano na mwanafunzi wa chuo cha CBE, Ludovick Angelino, ambaye ni mshindi wa tatu aliyejinyakulia shilingi laki tatu

MAMBO 10 KUHUSU DIAMOND LIKIWEMO LA KUMILIKI ZAIDI YA BILIONI MOJA KATIKA ACCOUNT YAKE

1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.
3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.
4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.
6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.
7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.
8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.
9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.
10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk.

CHECK OUT WEMA SEPETU PAMOJA NA MIRAJI KIKWETE WAKIWA NA KUNDI LA MAKOLE HEXAGON KUTOKA DODOMA:

ERICK MSHANA KULIA KATIKATI WEMA SEPETU PAMOJA NA MIRAJI






 BAADHI YA KUNDI LA MAKOLE HEXAGONI KUIA NI SUDI NA MSABAHA KUTOKA MAKOLE KULIA NI ROMA & MIRAJI 
MAKOLE HEXAGONI NI KUNDI LINALOWAKILISHA DODOMA PANDE ZA MAKOLE AMBAPO WALIKUWEPO WAKIWAKILISHA MAKUNDI YOTE KUTOKA DODOMA MAKOLE HEXAGON PAMOJA NA EAST ZUU CAMP:WEBSITE HII INAPENDA KUTOA PONGEZI KUBWA SANA KUNDI LA MAKOLE HEXAGON AMBAO WAMEWAKILISHA VEMA KATIKA SAFARI YA MWISHO YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU  NGWEA, PONGEZI ZIKUFIKIE  ERICK MSHANA KUTOKA VODACOM ,SUDI BOY PAMOJA NA MSABAHA BILA KUMSAHAU BUSHOKE KWA USHIRIKIANO ALIOTOA AKIWA SOUTH NA WENGINE WENGI WALIOWAKILISHA MJI WA DODOMA:

MAREKANI YAUNDA SHERIA KUWADHIBITI WANAUME WANAOVAA SURUALI CHINI YA MAKALIO YAO

Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo ambao bado wako shuleni.
Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza mitaani.
Sheria hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
Unaonaje sheria kama hii ikija Tanzania pia?

HATIMAYE NGWEA AZIKWA KWENYE MAKABURI YA KIBONDA MKOANI MOROGORO....HIZI NDIO PICHA ZA MAZIKO YAKE

Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.

Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri.

 
 Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.
16f11344cea711e2813a22000a1f8f34_7
75e8603ecea511e29ecd22000aaa08de_7
4406673ccea511e2850422000a1f9a85_7
“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.


Naye Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpk hapa tulipomsindikiza panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”
e1147594cea211e2a86422000a1f9839_7
ee9d94facea411e2a9ea22000ae81462_7
f18745b2cea411e2aa3022000a9e2931_7

KHADIJA KOPA AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE JANA KWA AJILI YA MSIBA WA MUMEWE JAFFARI ALLY

Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki.
Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.

TASWIRA KUTOKA MSIBANI KWA MAMA MZAZI WA JAFFARI ALLY (MUME WA KHADIJA KOPA)

 Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu nyumbani kwake Tandale jijini Dar.

 Simanzi na majonzi vilitawala msiabani hapo.
Akina mama waliofika kumpa pole Mama Mzazi wa Jaffari.

SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, Tandale jijini Dar. 

Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana  katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

 Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake mzazi ni Mwenyekiti wa UWT Tandale.


 Mungu ailaze roho ya marehemu Jaffari Ally mahali pema peponi. AMEN!