Baada
ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi
makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya
Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.
Kabla
ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake
kwenye uwanja wa Jamhuri.
Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa
heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika
Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao
wamehudhuria mazishi hayo.
“Marehemu
Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu
akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.
Naye
Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpk hapa tulipomsindikiza
panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”
Kesi ya Zumaridi yapangiwa hakimu mpya
-
Hakimu Monica Ndyekobora ameondolewa kusikiliza shauri la jinai namba
12/2022 linalomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wenzake
83 bad...
2 years ago