Pages

Friday, June 28, 2013

SHILOLE AMTIMUA MDOGO WAKE BAADA YA KUJAZWA MIMBA AKIWA MIKONONI MWAKE

STAA wa sinema za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtimua mdogo wake aliyekuwa akiishi naye aitwaye Mary baada ya kunasa ujauzito.
 

Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza habari kuwa, Shilole alifikia maamuzi hayo baada ya kumuonya binti huyo aachane na mwanaume aliyemjaza mimba hiyo lakini hakusikia hivyo akaona bora amtimue.
 
“Kamtimua baada ya kumuonya mara nyingi bila mafanikio akaona isiwe tabu bora aepuke aibu,” kilisema chanzo hicho.


Alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, mdogo huyo wa Shilole alikiri kutimuliwa na sasa amehamishia makazi kwa jamaa yake anayefahamika kwa jina la Tonny Montensi anayeishi Sinza, jijini Dar.