MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni huku nyingine akiwa chooni akikata gogo.
Picha
hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila
akasema ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika
hoteli ambayo hakuitaja jina.
Baadhi ya watu waliyoziona picha hizo
walimponda wakidai eti ni ulimbukeni lakini wapo waliomtetea kwa kusema,
ni staili tu ya maisha aliyoamua kuishi.
“Ushamba
tu, ndo nini sasa? alisema mmoja wa
wadau huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema:
“Msimuonee wivu mwenzenu, anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
Dida
alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi
na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana
anawawekea kwenye blogu yake.