Ni ukweli ulio wazi kuwa star wa ‘Kesho’ Diamond Platnumz ‘anaweza’
kuwa msanii wa Tanzania anayefanya show nyingi zaidi kwa sasa na za
gharama kubwa, baada ya kuwachanganya mashabiki wa Comoro na crew yake
ya Wasafi weekend iliyopita sasa anategemewa kushare jukwaa moja na
wakali kutoka Nigeria Davido na Ice Prince jijini Nairobi mwezi July.
Diamond Platnumz kipenzi cha mabinti ataungana na star wa Nigeria hit
maker wa ‘Dami Duro’ Davido, Ice Prince, Victoria Kimani wa Kenya, na
wakali wengine katika ‘Boombaataa Festival’.
Mtandao wa Ghafla umethibitisha ushiriki wa Diamond katika show hiyo
kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka nchini Kenya, yenye lengo la
kuleta burudani ya utofauti kwa wanamuziki wa Afrika, fashion pamoja na
utamaduni.
Show hiyo inategemewa kufanyika (July 27) mwaka huu Nairobi, Kenya.