MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu anayedaiwa kuwa alikuwa Mpenzi wa Ngwea aitwaye Misheily.
Mzungu huyo alionekana akilia kwa uchungu huku akitoa maneno
yaliyoashiria kuwa ameumia sana kuondokewa na ‘mtu’ wake huyo ambaye
huenda walikuwa na malengo mazuri ya baadaye.
Aidha, kilio alichokuwa akiporomosha binti huyo kiliwafanya watu
waliokuwa karibu naye kumsikitikia na kuzidishiwa majonzi kwani ilifika
wakati akaishiwa nguvu.