Mfanyakazi wa ndani aliyejiua kisa mapenzi aitwaye Devotha Sanga leo
ameagwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Marehemu Devotha alijinyonga Juni 4 mwaka huu akiwa nyumbani kwa bosi
wake eneo la Kitunda jijini Dar kwa wivu wa mapenzi.
Devotha alikuwa
katika penzi na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Christopher
anayedaiwa kuwa na wapenzi wengi kiasi cha kusababisha marehemu kuchukua
uamuzi huo.
Baada ya kuagwa mwili wa Devotha umesafirishwa kuelekea
Njombe kwa mazishi.