Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu nyumbani kwake Tandale jijini Dar.
Simanzi na majonzi vilitawala msiabani hapo.
Akina mama waliofika kumpa pole Mama Mzazi wa Jaffari.
SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala
nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa,
Tandale jijini Dar.
Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa
Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana
katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa
kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake mzazi
ni Mwenyekiti wa UWT Tandale.
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaffari Ally
mahali pema peponi. AMEN!