Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume
zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa
majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha
miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa
wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na
vijana wadogo ambao bado wako shuleni.
Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya
makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria
mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo
na kukatiza mitaani.
Sheria hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya
kuogelea na sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari
kuwa amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea
makalio nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
Unaonaje sheria kama hii ikija Tanzania pia?