STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa
vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi
wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi.
Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu
vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati
nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha
majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.
Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss
Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia
nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini
alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua
tatizo.
Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.
Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.
Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita
wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia
moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.
Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya
nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na
kuanza kutoa mkong’oto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele
yake.
Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio
la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni
isiyoandikika kutokana na ukali wake.