Mpaka sasa tayari tumeshuhudia couple 4 za housemates katika Big Brother ‘The chase’ , lakini couple ya mu Ethiopia Betty na mu Sierra Leon Bolt ndio ilikuwa ya kwanza kufahamika katika wiki ya kwanza toka mchezo uanze (May 26).
Couple ya Bolt na Betty ndio ilikuwa ya kwanza pia ku’kiss kama
uthibitisho wa ‘love at first sight’. Baada ya hapo maisha ya mjengoni
yaliendelea vizuri huku mapenzi ya ‘love birds’ hawa yakizidi kukua kila
kukicha japo waliamua kupeleka mambo taratibu.
Lakini wiki hii inaonekana kiu ya toka (May 26) iliwakaba ‘love
birds’ hawa na kuamua kuikata kwa kufanya kile wanachofanya wapenzi
wanapokuwa faragha (watu wazima naamini mnanielewa) yes , they did it!
Bolt iliifunga nut ya Betty usiku wa manane wakati washiriki wenzao
wakiwa wamelala!!
Ikiwa ni sehemu ya kujaribu kuyaokoa mapenzi yao, wiki hii baada ya
Betty kutwaa ukuu wa Diamond House (HOH) aliweza kupata mamlaka ya
kumuokoa mshiriki yeyote anayekuwa ameingia kikaangoni.
Hivyo aliitumia
nafasi hiyo kuliokoa penzi lake kwa kumuokoa Bolt ambaye alikuwa
amependekezwa kuingia kikaangoni, na kumchagua Feza Kessy wa Tanzania
aingie kikaangoni badala ya kipenzi chake.