Pages

Friday, June 28, 2013

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD RAIS OBAMA


Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi.



Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.


Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.


Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.