Afisa wa Vodacom akimueleimisha moja ya wateja waliojitokeza kupata huduma katika banda la Vodacom lililopo katika maonesho ya 37 ya sabasaba jijini Dar es Salaam, Kampuni hiyo sasa imewawezesha wateja wake kulipia bidhaa kupitia huduma ya M pesa katika maonyesho hayo.
Meneja wa Mradi wa kuwawezesha wananawake wa “MWEI” Grace Lyon akiwaelimisha baadhi ya wateja waliotembelea banda la Vodacom katika maonesho ya 37 ya sabasaba ,namna ya mradi huo unavyofanya kazi kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo wanawake kupata mikopo isiyokuwa na riba mradi huo hadi sasa umewawezesha wanawake zaidi ya 7,000.