Alianza kuonekana kwenye fashion mwaka 2012 kwenye maonesho ya Swahili Fashion Week chini ya mwanamitindo maarufu nchini Mustapha Hasanali, ameshiriki kuonesha mavazi kwenye Harusi fashion week iliyofanyika chini ya mbunifu wa mavazi Ally Rehmutula na pia alishawahi kushiriki na kushinda kwenye mashindano ya wanamitindo ya Maridadi model search yaliyofanyika hapa Tanzania.
Danny ni mwanasheria kitaaluma na ana degree ya sharia toka chuo cha Tumaini Iringa
Katika interview tuliyofanya naye hivi karibuni Danny amesema pamoja na kuwa mwanamitindo anamipango ya kuwa muigizaji kwani ni kitu alichokuwa anapenda kukifanya tangu utotoni.