skip to main |
skip to sidebar
SH. 500/- SASA ITAKUWA SARAFU BADALA YA NOTI ILI KUIFANYA ISICHAKAE HARAKA
KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake
kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.
Akizungumza
na gazeti la Tanzania Daima juzi kwenye viwanja vya maonesho ya
kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha,
Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni
na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa
na ubora wake.
Dollah alitaja sababu
nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na watu wengi
kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa kuzihifadhi
vizuri:
“Tofauti na noti nyingine kama vile zile za sh 5,000 na 10,000
hizi utakuta mara nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh 500 kwa sababu
noti hizi watumiaji wake wengi ni wale wenye akaunti benki.”