Vitendo vya wanafunzi kupigana exile( kumpisha room ili angonoke na mpenzi wake)
vimekuwa vikishika kasi ya ajabu katika hosteli za wanafunzi
wa vyuo vikuu mbalimbali ambao kwao limekuwa ni jambo la
kawaida...!!
Hali
imekuwa ni tofauti kidogo kwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapa
nchini ambaye yuko mwaka wa kwanza na anategemea kuingia mwaka wa
pili.
Akiongea na mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina , mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa Exile imemuathiri sana kisaikolojia.Imemfanya aishi kama mtumwa huku taaluma yake ikiyumba kwa kasi.
Hili ni simulizi la mwanafunzi huyo:
"Maisha
ya shule yana changamoto nyingi sana.Kwa mtu yeyote ambaye ni
mcha mungu ni lazima itamuwia vigumu sana kukabiliana na hali
hii.
"Nasema
hivi kwa sababu ndani ya hosteli huwa tunaishi watu tofauti
wenye malezi tofauti.Kasheshe ni kwetu sisi first year...
"Mazingira
kwetu ni mageni na ndani ya hosteli tunaishi na mabraza wa
miaka ya juu wenye wapenzi wao hapo hapo chuoni ambao huwaleta
vyumbani na wakati mwngine hulala nao.
"Wanapokuja
na wapenzi wao vyumbani ni lazima uwapishe wafanye mambo
yao.Na ukiwapisha maana yake utoke kwa zaidi ya masaa matatu
mpaka matano
"Ndani
ya chumba changu tulikuwa tunaishi watatu, mmoja mwaka wa pili,
mwingine wa tatu na mimi mwaka wa kwanza.Wote hao walikuwa na
wapenzi wao hapo hapo chuoni.
"Siku zote za wikiendi walikuwa wamezigawana.Mmmoja ilikuwa ni jumamosi na mwingine jumapili.Yaani
kwa kifupi ni kwamba sikuwa na uhuru wa kukaa chumbani siku
za wikiendi na wakati mwingine hata siku za wiki.
"Nimeamua
niwe muwazi maana hali hii imekuwa ni kero kwangu na imekuwa
ikiniathiri sana kisaikilojia na kusababisha taaluma yangu
iyumbe nikilinganisha na nilipokuwa naanza.
"Naomba
nitoe ombi kwa wanafunzi wenzangu.Sote tuko vyuoni kutafuta
maisha na zile hosteli tunazilipia kwa gharama sawa.Kwa nini
umsumbue mwenzako wakati gesti zipo?..Yangu ni hayo tu"
Kesi ya Zumaridi yapangiwa hakimu mpya
-
Hakimu Monica Ndyekobora ameondolewa kusikiliza shauri la jinai namba
12/2022 linalomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wenzake
83 bad...
2 years ago