Pages

Monday, July 15, 2013

WEMA: SIACHI MKOROGO HADI MADUKA YAFUNGWE

THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe. 
 
Wema katika pozi linaloonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika.
Baada ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu’ kuulizwa na kujibu hivyo wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa BBM zikimuoneshaakiwa nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi kwenye mwili wake.
..Mapaja ya mrembo huyo.
Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.

Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.
Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.