Pages

Thursday, February 28, 2013

Baada ya Maisha Yake Kuwa Hatarini Tena, Rick Ross Aongezewa Ulinzi Na Polisi...


Rapper kutoka Label ya Maybach Music Group [MMG], Rick Ross ameongezewa ulinzi na jeshi la polisi la New Yorkbaada ya rapper huyo kupata vitisho vya kuuwawa tena kutoka kwa watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa TMZ, rapper Rozay huyo atakuwa na ulinzi wa Masaa 24 kutoka kwa polisi hao wa NY.
Ross anaetamba kwa sasa na album yake ya GOD FORGIVES I DONT na pia mixtape BLACK BAR MITZVAH yupo katika maandalizi ya album yake ya 4 inayokwenda kwa jina la MASTERMIND.

Mtandao Wa Google Waja Na "GOOGLE GLASS"... Hii Kali Ya Mwaka...

Tukiongelea neno GOOGLE basi natumaini kila mtu atakuwa anaelewa hasa kwa wale watumiaji wakubwa na wa mara kwa mara wa Internet.
Sasa mpya kutoka kwenye kampuni hiyo ya Google ni kuwa imetoa bidhaa mpya ambayo ipo katika mtindo wa Miwani (Google Glass) yenye uwezo wa kurekodi video na kupiga picha mahali popote utakapo kuwepo.
Google ndio kampuni ya kwanza kuja na Teknolojia hiyo ambayo ni rahisi sana kuitumia.
Imetengenezwa katika mtindo wa kuiamrisha (Command), unachotakiwa kufanya ni kusema ''Ok Glass Take A Picture'' nayo itafanya hivyo na pia itakupa uwezo wa ku-share picha hiyo kwa marafiki, ndugu, washkaji zako papo hapo.
Pia unaweza kuitumia miwani hiyo kwa Video Chat kama ilivyo Skype, pia unaweza kutafuta habari kupitia google, kutasfsiri lugha na mengineyo.
Unaweza kufanya yote hayo bila kutumia mikono yako, kwa nchini Tanzania kifaa hiki kinakadiriwa kuuzwa kwa bei ya Shilingi Millioni 2.2 ambazo ni sawa na dola $1500 za kimarekani.

Behind The Scene Ya Video Ya Young Killer ''DEAR GAMBE''...


Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka MWANZA, ambaye hivi sasa yupo chini ya usimamizi wa Producer Mona Gangsterkutoka Classic Records, Young Killer ambae anatamba na ngoma yake ya Dear Gambe ambayo amemshirikishaBelle 9, sasa yuko mbioni kuachia kichupa cha ngoma hiyo.
Young Killer ambae ni mmoja wa washindi wa shindano la SUPER NYOTA ya FIESTA (2012) kutoka MWANZA, ana-shoot video hiyo chini ya Director Mejja kutoka SEAN ENT.
Jamaa wame-shoot video hiyo maeneo tofauti tofauti ya jijini Dar na updates ni kwamba inatarajiwa kutoka siku za hivi karibuni.

Wednesday, February 27, 2013

MAGAZETI YA AFRKA YAPOTOSHWA KUHUSU HABARI ZA MIKE TYSON KUBADILISHWA KUWA MWANAMKE


Tarehe 12/12/2012   iligeuka kuwa siku ya wajinga duniani badala ya April Mosi baada ya magazeti mengi ya Afrika na hasa Tanzania kuingizwa mkenge na habari ya kubuni ya Mike Tyson kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke. 

Bahati mbaya sana ni kuwa bado watanzania wengi yakiwemo magazeti na hata baadhi ya vituo vya radio vimeendelea kuisema habari hiyo ya kupotosha kama vile ni ya kweli.


Habari hiyo hata hivyo iliandikwa mwishoni mwa mwezi November na website ya nchini Uingereza ambayo huandika habari za kubuni iitwayo NewsBiscuit.

Magazeti maarufu nchini yakiwemo Mwananchi na Jambo Leo yaliiandika habari hiyo pamoja na magazeti mengine makubwa barani Afrika kama The Standard la Zimbabwe na website ya Ghana SpyGhana.

Kwa mujibu wa BBC,NewsBiscuit ilidaiwa kuelemewa zaidi jana kutokana na wasomaji kuwa wengi kutoka Afrika.

“Tumepata wasomaji zaidi ya nusu kutoka Afrika katika siku chache zilizopita ambao tungetegemea kuwapata kwa mwezi mzima,” mwandishi wa mtandao huo John O’Farrell aliiambia BBC.

Alisema habari hiyo ilisomwa zaidi ya mara 50,000 katika siku chache tu ikiwa ni mara 20 zaidi ya kawaida.


VIDEO ZA MZIKI WA MTOTO WA MIAKA 9 ZALETA BALAAA


Mtoto mwenye umri wa miaka 9, Luie Rivera Jr., ambaye jina lake la kisanii ni “Lil Poopy,” ameonekana kwenye video anazozipost online hususan kwenye mtandao wa YouTube, akicheza muziki na wasichana wakubwa kwa umri wake, akiendesha magari ya kifahari kama Ferrari na akirap maneno kama “coke is not a bad word.” 


Katika video nyingine mtoto huyo anaonekana akicheza na msichana katika pozi chafu huku watu wakimtupia hela. 
poopyladies
Idara ya polisi ya Brockton, Massachusetts, imewasiliana na ofisi inayoshughulikia masuala ya watoto na familia nchini humo baada ya kupokea simu nyingi kutoka kwa watu walioguswa kufuatia kuona video zake.
lil-poopy-584x350
Baba wa rapper huyo Luie Rivera ameajiri mwanasheria kujilinda na uwezakano wa kukamatwa kwa kosa la jinai.

Tazama video hii ya remix ya wimbo wa French Montana.

MSANII AMTELEKEZA MTOTO STENDI YA UBUNGO


MREMBO aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3). 

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.


Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.


“Maya amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na amekuwa akimjali sana kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka alimwambia Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto) akasalimie, Maya akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha (nyumbani kwao) ndipo waende Bukoba.


“Justine akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda Arusha na kuna watu walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam, wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata, siku iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba kwa mama yetu (bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia kondakta,” alisema Monalisa na kuongeza:

“Alikubaliana na kondakta huyo kisha akamwachia namba ya simu ya mama na yake ili waweze kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.


Kwa bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka siku inayofuatia. Mtoto akaanza kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi mzuri.


“Bahati nzuri mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na kuonana na huyo konda, akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana naye, kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua kuchukua jukumu la kusafiri naye.”


Monalisa alikubali kutoa namba za simu za msamaria aliyejitolea kusafiri na mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .


“Mimi kama mzazi iliniuma sana kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi bila uangalizi. Nilishangaa sana kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje kumwacha mwanaye mdogo namna ile asafiri mwenyewe?” alisema.



Risasi lilimtafuta baba mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye Marekani ambapo alisema: “Jambo hilo limeniumiza sana. Kwa kweli kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo) ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria.

“Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama Bukoba.”


Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua kioja baada ya kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo na pia akadai eti hana mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake yote.

Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito.

MSANII OMOTOLA ANG'AA HOLLYWOOD


Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise

Man Water Amjibu Steve RnB Kwa Kutumia Beat Ya Jambo Jambo, "NAWAOGOPA"...


Producer maarufu kutoka studio ya Combination Sound, Man Water ametoa track yake inayokwenda kwa jina la''NAWAOGOPA''.
Katika ngoma hiyo, mdundo [beat] uliyotumika ni ule wa BUSY SIGNAL - COME OVER ambao pia, Steve RnBameutumia kama sample katika ngoma yake mpya ya Jambo Jambo.
Sikiliza ngoma yeyewe hapa chini:

ILE VIDEO YA WIZKID – AZONTO NDIO HII

Ni mkali wa Nigeria ambae amekuwemo kwenye headlines kwa kipindi kirefu kidogo sasa hivi kutokana na stori zake za kuachana na lebo iliyokua inamsimamia na kuanzisha lebo yake mwenyewe, pamoja na hayo… mpaka sasa sijaelewa ile dili yake ya kuwa chini ya Akon iliishia wapi lakini kwa sababu connection yangu ni nzuri na wakali wa Nigeria, nitaifanyia kazi hii ishu.

Check Mambo Yalivyokuwa Kwenye London Fashion Week...


Kama ulimiss kuona lile tamasha la London Fashion Week 2013 ambalo lilifanyika wiki iliyokwisha, yaani tarehe 15 hadi 19 mwezi huu.
Tanzania ilibahatika kuingia katika Kumi Bora katika tamasha hilo kubwa duniani.
Check yaliyojiri kwenye tamasha kupitia video hii hapa chini...

Chris Brown Na Rihanna Kufunga Ndoa Ifikapo July Mwaka Huu...???


Mastar wawili kutoka nchini Marekani, Chris Brown na mpenzi wake Rihanna wameripotiwa kupanga kufunga ndo ifikapo July mwaka huu.
Jarida moja maarufu sana la nchini Marekani liitwalo ''Star Magazine'' limeripoti kuwa mastaa hao wana tarajia kufunga ndoa ifikapo July mwaka huu katika visiwa vya Barbados.
Kwa mara ya kwanza wawili hao wamepanga kufunga ndoa hiyo ambayo itakuwa ya kitofauti ikiwa na watu wa karibu ambao wanaamini Chris Breezy amebadilika kweli na upendo wa dhati kwa Rihanna hasa baada ya tukio alilolifanya mwaka 2009.
Mwaka 2009, Chris Brown alimpiga mwanadada Rihanna na ku-make headlines kubwa sana iliyopelekea watu wengi kumchukia ikiwemo kushtakiwa kutokana na kitendo hicho.

Behind The Scene Ya "FREAKS" French Montana ft. Nicki Minaj ... Nicki Is That Girl Yo'...

Rapper French Montana ambae yuko chini ya label ya Bad Boys sasa yuko mbioni kuachia video ya ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha femcee kutoka kundi la Young Money [YMCMB], Nicki Minaj.
Ngoma hiyo ikiitwa "FREAKS" it shows parts of the video, where Nicki on this corridor and actually how she can befreeakyyy... Lol.
Check the video hapa chini mtuangu...

Tuesday, February 26, 2013

[PHOTO] Kanye West Na Kim Kardashian Watokea Kwenye Front Cover Ya L'Officiel Hommes..


Stars wawili ambao ni wapenzi wanaotarajia kupata mtoto, Kanye West Na Kim Kardashian wameonekana wakiwa wametokea kwenye jarida maarufu la ''L'Officiel Hommes'' la nchini Ufaransa.
Wapenzi hao wameonekana kwenye ukurasa wa mbele kabisa wa jarida hilo huku wakiwa kukumbatiana. Jarida hilo linatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Brand New: Ngwair ft. TID - NO BEEF...

Ile ngoma tuliyoiongelea earlier, its now here!!! Ni ngoma mpya kutoka kwa Cowwizzyy kutoka East Zoo akimshirikisha mwanae wa karibu TID "Mnyama" ikijulikana kama NO BEEF...
NO BEEF ni moja ya ngoma za Ngwair tukiongelea Denja Vu Music, yeah DENJA VU MUSIC, its a new thing presented by Ngwair and its the beginning.... Ngwair in the store room.
Ni mpya ikiwa imepikwa na Joff Master, producer kutoka B Records... Kama unakumbuka vizuri JOFF MASTER ndiye producer aliyechapa "120" ya Ngwair akimshirikisha Chiddi Beenz enzi hizo ikiwa ni KAMA KAWA RECS.This is the new joint itself, isikize na kui-download hapa chini:

Huyu Ndiye Mchumba Wa Linex Alievalishwa Pete Ya Uchumba..

Mwanamuziki wa kizazi kipya anaetamba na ngoma yake mpya ya MAHAKAMA YA MAPENZI, Linex amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake.
Linex ambae pia anatamba na ngoma zake kama Moyo Wa Subira, Mama Halima, Ngekewa, Aifola na nyingine nyingi amemvalisha pete wakiwa waili tu mchumba wake huyo mweye asili ya Finland anaefahamika kwa jina la Suvi.
Linex amechukua uamuzi wa kufanya kitendo hicho kwa siri kwa sababu ameona haikuwahusu watu wengi wajue maana ni kitu ambacho kinawahusu wao wawili tu.
Check picha zaidi za wawili hawa pamoja na pete yenyewe:

HILI NDIO GARI LILILONUNULIWA NA MCHEKESHAJI STAA WA NIGERIA, ALITOA ODA KIWANDANI.


.Huu ndio mkoko mpya ambao model yake ni ya 2013, ni Opel Insignia na bei yake ni pound elfu 42.
2013 unazidi kuwa mwaka wa mastaa wa Nigeria kununua magari ya kifahari na yaliyotengenezwa hivi karibuni ambapo leo kwenye headlines muhusika mkuu ni mchekeshaji aitwae Basket Mouth akiwa ni staa ambae Nigeria imemfahamu kutokana na uchekeshaji wake.
Imeripotiwa na Linda kwamba hili gari Basket alitoa oda kiwandani na hakuna gari kama hili Africa ikiwa ni siku chache tu amelinunua baada ya kukamilisha ujenzi wa hii nyumba hapa chini ya mamilioni ya Naira zawadi kwa mama yake mzazi maarufu kama Madam Okpocha.

Wow!Nicki Minaj's


Nicki Minaj surprised many when she stepped out in a white dress and toned down look for the launch of her lipstick line at the MAC store in Beverly Hills.
I agree with a million others,she has never looked more beautiful.Please she should stick to this fresh look.

Monday, February 25, 2013

SIKILIZA U HEARD NA GOSSIP COP


leo hii kupitia kwenye u heard ya gossip cop, inamuhusu muigizaji na mchekeshaji Steve Nyerere...inasemekana agongwa na gari lake na mwisho wa siku ajikuta lupango, baada ya kupigwa bonge la tanganyika jeki.......isikilize hapo chini 

HII NDIO SABABU YA ''Kama Zamani'' Ya Mwana FA Kutoachiwa Leo Kama Ilivyotangazwa...


Ile track ya ''Kama Zamani'' kutoka kwa rapper Mwana FA ambayo ameshirikiana na Kilimanjaro Band [Wananjenje] pamoja na Man'dojo na Domokaya ambayo ilitakiwa kutoka leo imeahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Lifeline Music Inc. ndio kampuni inayosimamia kazi zote za rapper huyo, na ndiyo iliyotoa taarifa hizo za kuahirisha kwa uzinduzi wa ngoma hiyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.
Soma taarifa kamili hapa chini:
TAARIFA KWA WADAU

Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya. Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wananjenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi.

Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.

Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.

Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.

Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu piakuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro Band(WanaNjenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama Zamani kama ilivyopangwa hapo awali.

Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.

Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.

Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.

Henry Mkumbukwa
PR Strategist
Lifeline Music Inc.
Fans wengi wamekuwa wakiisubiri track hii kwa hamu, tumekuwa tukiombwa links na wengi wakiiulizia kwa shauku ya kuusikia, Lifeline Music wamezungumza na kuweka bayana kilichotokea.
I think its a good deal they are trying to pull through, tusubirie tuone lini itatoka. As we promised ikitoka tu utaipata hapa hapa...
MAMBO MAZURI HAYATAKI HARAKA... Lol.. One!!

Show Ya AliKiba Na Ommy Dimpoz Ilivyofanyika London, Uingereza...


AliKiba na Ommy Dimpoz wapo nchini Uingereza wakipiga show kwa mashabiki wao waishio nchini humo.
Hii ni moja ya show ambayo waliifanya weekend hii katika ukumbi wa disco uitwao OutLet.
Check baadhi ya picha za kwenye show hiyo, tazama hapa chini...

Timbulo Ashukiwa Kukamatwa Na Madawa Ya Kulevya...


Msanii wa kizazi kipya maarufu kama Timbulo ambae anatamba na baadhi ya ngoma zake kama Domo Langu, WaleoWakesho, Samson Na Delila na ngoma hizo kumfanya atambulike zaidi katika tasnia hii ya muziki inasemekana amekamatwa na madawa ya kulevya.Kuna tetesi kuwa msanii amekamatwa mjini Bujumbura, Burundi kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya.Timbulo alikuwa nchini humo akiwa anafanya shows mbalimbali. Bado tunaendelea na kufuatilia taarifa kamili juu ya habari hii.

Show Ya Q Chillah Pale Maisha Club Siku Ya Jana...


Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kupiga show, mwanamuziki Q Chillah alipiga bonge la show katika ukumbi wa disco wa New Maisha Club jana.
Q hakuwa mwenyewe kwani alisindikizwa na wasanii wengi kama H-Baba, Banza Stone, Ally Nipishe, Canal Top, Beka kutoka THT pamoja na Cassim Mganga.
Pia moja ya matukio yaliyosisimua watu wengi katika show hiyo ni pale Q Chillah alipopanda jukwaani pamoja na baba yake ambae zamani alikuwa ni mchezaji mpira, Mzee Shaban Katwila.
Check baadhi ya picha za kwenye show hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo...