Kwenye jarida la mwezi November la Bongo5, AY alikuwa mmoja ya wasanii tuliowaweka kwenye orodha ya ‘Bongo Kings’ hivyo si jambo la kushangaza kuona jarida la Heshima la Kenya kumweka kwenye orodha yake ya ‘2013 Hip Hop Heavyweights’. AY ambaye jina lake halisi ni Ambwene Yessaya ana mengi aliyoyafikia na kumfanya apate heshima.
Tukianza na tuzo ya Channel O aliyoipata mwaka jana (Video bora ya Afrika Mashariki) kwa wimbo wake ‘I don’t wanna be alone’. AY ndiye msanii wa Tanzania ambaye video zake zinachezwa zaidi kwenye TV za kimataifa, Speak With Your Body, Party Zone, Money na list inaendelea.
Pia anang’ara kwenye video aliyoshirikishwa na msanii wa Nigeria Goldie Harvey’Skibono’. Tayari ana wimbo uliokamilika aliofanya na Sean Kingstone, so bado tu una wasiwasi na uheavy weight wa Ambwene?
Kampuni yake ya Unity Entertainment imeendelea kukua na sasa ikiwa na wasanii kama Ommy Dimpoz, Feza Kessy na Stereo kwenye roaster yake.