Imekuwa zaidi ya saa 24 tangu kifo cha Goldie Aliyekuwa mshiriki wa Big brother africa house mate, Aliyekuwa mumewe Andrew Harvey ameibuka na picha zao za ndoa na picha nyingine ambazo zimepigwa hivi karibuni wakiwa pamoja kama mke na mume . Andrew pia kupitia ukurasa wake wa facebook amemuomba mwanamuziki wa kenya Prezzo katika wakati huu mgumu "kuacha familia yao ihuzunike kwa amani"
Katika mahojiano na TheNetNG, Andrew pia alithibitisha kwamba yeye an Goldie waliowana mwaka 2005, yeye na Goldie walikuwa mke na mume hadi kifo chake.
"uhusiano" na Prezzo ulikuwa ni mchezo tu kwa ajili ya TV - "Prezzo ilikuwa sehemu ya BBA mchezo, kama vile katika sinema, alisema Andrew sikuwa na wasiwasi wowote ule
Aliendelea kusema kuwa yeye na Goldie hivi karibuni Krismasi likizo iliyopita walikuwa pamoja pamoja Malaysia, na mara ya mwisho kuzungumza na mkewe ilikuwa siku ya Valentines day
Na kama tunavojuwa mpaka kifo chake Goldie alikuwa anatumia jina la ukoo la Andrew - Harvey.
ukurasa wa facebook ya Andrew Harvey









