Alizaliwa mwaka 1945 tarehe kama ya leo, jina halisi Robert Nesta Marley katika kijiji cha Nine Mile ndani ya Saint Ann Parish, Jamaica. Baba yake [Norval Sinclair Marley] alikuwa mtu mweupe kutoka Sussex, England huku Mama yake akiwa mweusi Cedella Booker, Jamaica.

Akijulikana zaidi kama
Bob Marley, muimbaji na kiongozi wa Kundi la
Reggae la
The Wailers lililoundwa mwaka
1963,alikuwa na upigaji gitaa mzuri aliokuwa anafanya ikiwa ni pamoja na kuimba kwa harakati kupitia muziki wa
Reggae na amekuwa maarufu sana kupitia muziki huo akisambaza harakati duniani kote.
Bob Marley Akipiga Show Huko Italy, Mwaka 1980.
Bob amebakia kuwa mwanamuziki mkubwa sana aliyewahi kutokea akiwa bado anaishi mioyoni na akilini mwa watu aki-inspire wanamuziki wengi, wanaofanya reggae na wasiofanya aina hiyo ya muziki pia... He trully A LIVING LEGEND!
Happy Birthday Bob Nesta Marley.