Pages

Monday, February 4, 2013

TIMBULO SASA MIKONONI MWA ROSE NDAUKA ...

Ali Timbulo
Timbulo msanii wa muziki na Filamu Swahiliwood.

Baada ya kutesa kwenye anga ya muziki, msanii mahiri wa muziki wa Bongofleva nchini, Ally Timbulo, ameanza safari mpya kwenye tasnia ya filamu, huku wadadisi wa mambo wakisema msanii huyo anafuata nyayo za msanii wa kike Jack ambaye alikuwa mpenzi wake siku za nyuma.

Timbulo ambaye hivi sasa anatesa na wimbo wake wa Bado Kijana, tayari ameanza kazi ya upigaji picha wa filamu kali nay a kusisimua iitwayo World of Benefit.Ali Timbulo Rose Ndauka

Timbulo akiwa na mwigizaji mahiri katika filamu Rose Ndauka moja ya scene za filamu hiyo
.Seleman Mkangara, Selles Mapunda.Watalaam chini ya Madirector Selles na Mkangara wakiwa makini kufuatilia filamu ya World of Benefit.
Rose Ndauka, Alli Timbulo
Timbulo akiwa na Rose kitandani katika filamu ya World of Benefit
Ndani ya filamu hiyo msanii huyo anapambana na wakongwe wa tasnia hiyo ya filamu kama Mohamed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mama Mjata, Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka na Awadhi Saleh ambaye anakuja juu katika tasnia ya filamu kwa sasa.
“Nimepata bahati kufanya kazi na wasanii wakongwe, lakini pia nimepata bahati ya kusimamiwa na maproducer mahiri kama Selles Mapunda na Seleman Mkangara, hivyo naamini itakuwa kazi bora” alisema Timbulo.
Filamu ya World of Benefit imetayarishwa na mtayarishaji wa filamu Hamees Suba ‘Kemikali’ na inaongozwa na Selles Mapunda ‘Director of Directors’, akisaidiwa na Suleiman Mkangara ‘Striker’ kwa upande wa upigaji picha wapo wataalamu kutoka Bollywood chini ya kampuni ya Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam.