Mdoli huyo mwenye thamani hiyo, akiwa ametengenezwa na kupambwa sehemu kubwa kwa almasi, alinunuliwa na wanandoa hawa kama zawadi kwa Blue ambaye ametimiza mwaka mmoja jumatatu iliyopita toka kuzaliwa kwake.
Barbie Doll amekuwa ni sehemu tu ya furaha hii, kwani pia Jay-Z na Beyonce wamemuandalia mtoto wao sherehe kubwa Blue Ivy ambayo inagharimu pauni za kiingereza 60,000 na cake yake ya birthday yenye thamani ya pauni 1,500 za kiingereza. Jay-Z na Beyonce wameripotiwa kutokuwa na tatizo katika kumfanyia mtoto wao huyo chochote kitakachoweka alama katika maisha yake yote ambapo kwa sasa wanatambulika duniani kama ma-star wanaolipwa hela nyingi pamoja katika mahusiano yao. Jay-Z Na Beyonce wanalipwa dola za kimarekani 78 milioni kwa mwaka.Jay-Z na Beyonce wamekuwa kwenye maandalizi haya ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa mtoto wao kwa wiki kadhaa sasa... just to make the best of it.