Pop & R&B Star Justin Bieber amewashangaza mashabiki wake walioshindwa kutafsiri nini chanzo cha haya yote anayoyafanya sasa, hasa baada ya kutupia picha inayomuonesha kwa upande nyuma akiwa ameshusha nguo yake akiwa na lengo la kuonesha makalio yake.
Bieber alitupia picha hiyo kwenye mtandao wa picha wa Instagram na baadae kuifuta, lakini ilionekana kuchukuliwa tayari maana iliendelea kuzagaa katika mitandao tofauti.Mwimbaji huyo ambaye sasa amefikisha umri wa utu uzima, amefanya hivi na kuwashtua wengi ambao walikuwa bado wanashangaa picha ya Bieber aliyokuwa akichoma kilevi aina ya bangi kwenye chumba cha hotel akiwa na washkaji zake akiwemo rapper Lil Twist.
Kwa haya matukio mawili ya haraka haraka unaweza kujiuliza ni bangi?? au ni umri, hela zinazopelekea kuwa huru kufanya chochote?!!...