Pages

Saturday, February 2, 2013

MAMA SHARO AMKANA MKAMWANA NA AELEZA SABABU YA KUUZA GARI LA MWANAYE

MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake. 


Akizungumzia  suala la gari, Mama Sharo amesema: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.

“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”


Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.


Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake.