Pop Star kutoka Marekani, Miley Cyrus juzi kati ametimba studio na rapper kutoka kundi la Taylor Gang, Wiz Khalifa kurekodi ngoma pamoja. ngoma hiyo ambayo itakuwa katika album ya Miley ijayo imetengenezwa na Producer mkali na kufanya vizuri sana miaka ya karibuni Mike Will.
Mbali na kufanya collabo na wanamuziki hawa, anazidi kuwashtua fans wake kutokana na kwamba Miley Cyrus anafanya aina ya muziki [genre] ya Pop lakini mwenyewe alisema hafanyi aina hiyo ya muziki ila ni katika kujaribu kufanya tofauti na wala hajaribu kuwa kama Rihanna au Nicki Minaj, hiyo sio aina yake ya muziki
.
Mike Will na Miley Cyrus
Miley ameshafanya tracks kadhaa na Mary, J., Lil Kim, Tyler The Creator na wasanii wengine ambao wanafanya aina ya muziki wa Hip-Hop.