Pages

Monday, February 11, 2013

Toni Braxton Aacha Kurekodi Muziki..

Mwanamuziki wa RnB wa muda mrefu kutoka Marekani, Toni Braxton amezungumza na kusema ameacha kurekodi muziki. Akizungumza katika moja ya talk shows kubwa Marekani, Toni amesema amechoka na amekuwa hana mapenzi ya karibu tena ya kurekodi muziki.
Toni ambae miaka ya 1990 aliwahi kutamba sana na nyimbo zake kama Breathe Again na Unbreak My Heart na kujichukulia Tuzo 6 za Grammy alisema ameacha kabisa kurekodi albums ingawa bado anafanya show za hapa na pale.
Katika interview hiyo Toni [mwenye miaka 45] aliongeza kuwa amegeukia kwenye maigizo na kwa sasa akiwa kwenye show ya TV ya Braxton Family Values na pia anafanya show nyingine inayoitwa "Twist Of Faith" itakayoanza kurushwa kwenye TV mwezi huu.