Pages

Monday, February 11, 2013

Swahili Fashion Week - Zanzibar Showcase Mwezi Huu...


Katika kuendeleza tasnia ya sanaa ya ubunifu na kuchangia maendeleo ya tasnia ya wanamitindo nchini Tanzania,Swahili Fashion imeandaa onyesho la mavazi Africa Mashariki na Kati litakalofanyika visiwani Zanzibar siku ya Tarehe15/2/2013 katika viwanja vya Mbweni Ruins.
Katika tamasha hilo wabunifu zaidi ya kumi watakuwepo kuonyesha mavazi yao huku wakitangaza dhana nzima ya kujali vitu vinavyotengenezwa Africa hususani Tanzania ili kuitangaza nchi ya yetu na rasilimali zote.
Hayo yalisemwa na muanzilishi muandaaji wa Swahili Fashion Week, Bw. Mustapha Hassanali wakati akielezea mikakati ya onyesho hilo ikiwa ni kutangaza na kuinua vipaji vya wabunifu wa hapa nyumbani.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa onyesho hilo litawashirikisha wabunifu ambao ni wazuri kutokea bara na visiwani ili kuonyesha ubunifu na ladha tofauti za kiutamaduni.