Star wa single ya "Whip My Hair", Willow Smith aamua kuuacha ulimwengu wa muziki na sinema kwa sasa. Willowambae ni mdogo wa Jaden, wakiwa ni watoto wa ma-star wa Hollywood, Will Smith na Jada Pinkett-Smithamechukua uamuzi huo na kumwambia Baba yake [Will] kuwa anataka kupumzika kwa sasa na kufurahia umri wake.
Willow, mwenye miaka 12 sasa, amewahi kufanya vizuri sana pale alipoanza kuimba na kutoka na track yake ya kwanza ya "Whip My Hair" iliyofanya vizuri sana katika ulimwengu wa muziki huku hivi karibuni akichukua nafasi ya kuigiza katika movie inayokuja ya "Annie".