kutoka Nigeria, Goldie Harvey famously known as "Goldie" anataraji kutengeneza album ambayo itagusa kila kona ya Africa. Goldie ambae pia alikuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa la mwaka jana ameyasema hayo katika interview aliyofanya na MTVBase Africa hivi karibuni.
Katika kufanikisha hilo, Goldie anataraji kufanya album hiyo ambayo bado hajaipatia jina na atleast wasanii 10 bora kutoka Africa ambapo mpaka sasa ameshafanya singles tatu ambazo zitatangulia, ikiwemo SKIBOBO featuring AY (@AyTanzania) kutoka Tanzania, MILIKI feat. Navio kutoka Uganda na GIVE IT TO ME akimshirikisha J.Martinskutoka Nigeria.
Goldie amekuwa akifanya vizuri sana kwenye muziki hasa baada ya kutoka kwenye Jumba la BBA-StarGame mwaka jana, ngoma zake zikisikilizwa sana Africa na duniani pia.