Pages

Thursday, February 7, 2013

Harusi Ya 2Face Idibia Kufanyika Dubai Mwezi Ujao...


Hatimaye ile ndoa ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Nigeria, 2Face Idibia na mchumba wake Annie Macaulay Idibia sasa inatarajiwa kufungwa Tarehe 23 March mwaka huu.
Masaa machache yaliyopita, Annie aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa ndoa hiyo itafungwaDubai.
Annie na mumewe mtarajiwa walikwenda Dubai kuangalia ukumbi ambao watakaofanyia harusi hiyo. Pia wawili hao wamepanga kusafiri baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wao wa karibu wa kuweza kuhudhuria harusi hiyo ambapo mpaka sasa 2face ameshazuia vyumba kadhaa katika hotel ya Bur Al Arab, Dubai.
Baadhi ya mastar kutoka Nigeria ambao watahudhuria harusi hiyo ni Don Jazzy, D'banj, Banky W, P-Square  na wengine wengi.