Msanii maarufu wa kizazi kipya, Dayna ambae anatamba na baadhi ya ngoma zake kama Mafungu Ya Nyanya, Nivute Kwako na nyinginezo sasa yuko mbioni kuachia track yake nyingine mpya ambayo inakwenda kwa jina la ''LEO''.
Leo ni track mpya ambayo amempa shavu Mr. Blue a.k.a Kabyser, star wa muziki huu wa Bongo Flava anaefanya vizuri pia katika tasnia hii ya muziki.
Fans wa Dayna kaeni tayari kwa ujio mpya kutoka kwa msanii huyo..