Pages

Friday, June 28, 2013

WEMA SEPETU APOTEZA MVUTO....MIKOROGO YAMUATHIRI....MICHIRIZI YAANZA KUPANDA USONI

Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri  wema  Sepetu  ambaye  ni  miss Tanzania  2006..
Wema  ambaye umri wake bado  haujamtupa  , hivi  sasa  anakabiriwa na tatizo la  ngozi  kutokana  na michirizi  kusambaa  mwili mzima  hasa  mapajani....
 Kamera  zetu  si  mara  ya  kwanza  kumshuhudia  Mrembo  huyu  akizingirwa  na  uzee  kwani  miezi  kadhaa  nyuma  tuliwahi andika  habari  inayofanana  na  hii  lakini  ikielezea  zaidi  michirizi  ya  mapajani....
Tofauti  na  hivyo, hivi  sasa  michirizi  hiyo   imekimbilia  kifuani  na  mabegani  hali  inayoashiria  kwamba  siku  si  nyingi  itahamia  usoni...
"Ukweli  Wema  Sepetu  sasa  amebaki sura  tu,mwili  umemtupa  kabisa .Nadhani  hii  yote  inatokana  na  matumizi  mabaya  ya  mikorogo"...alisema  shuhuda  mmoja  akimtazama  Wema sepetu  aliyekuwa  jaji  katika  shindano  moja  la  umiss  jijini  Dar

Baada  ya  kumsikia  shuhuda  huyo  akimtoa  kasoro  mrembo  huyo, mwandishi  wetu  alitinga  nyumbani  kwa  Wema  Sepetu  kufanya  naye  mahojiano  juu  ya jambo  hili
Alipofika  nyumbani  hapo, mwandishi  wetu  aligonga  geti  na  kufunguliwa  na  dada  mmoja  ambaye  alidai  kuwa  maadam Wema  alikuwa  amelala  na  kwamba  hawezi  kuamshwa mpaka  aamke  mwenyewe..

Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine barani ulaya. "Yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz Alipoulizwa kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema "aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa?

Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine barani ulaya.

"Yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz 

Alipoulizwa  kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema 

"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa?

OMMY DIMPOZ APATA SHAVU LA KUFANYA TOUR MAREKANI NA CANADA

Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine barani ulaya.

"Yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz 

Alipoulizwa  kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema 

"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa?

DIAMOND PLATNUMS KUPERFORM JUKWAA MOJA NA WAKALI WA NIGERIA NCHINI KENYA MWEZI UJAO

Ni ukweli ulio wazi kuwa star wa ‘Kesho’ Diamond Platnumz ‘anaweza’ kuwa msanii wa Tanzania anayefanya show nyingi zaidi kwa sasa na za gharama kubwa, baada ya kuwachanganya mashabiki wa Comoro na crew yake ya Wasafi weekend iliyopita sasa anategemewa kushare jukwaa moja na wakali kutoka Nigeria Davido na Ice Prince jijini Nairobi mwezi July.
Diamond Platnumz kipenzi cha mabinti ataungana na star wa Nigeria hit maker wa ‘Dami Duro’ Davido, Ice Prince, Victoria Kimani wa Kenya, na wakali wengine katika ‘Boombaataa Festival’.
Mtandao wa Ghafla umethibitisha ushiriki wa Diamond katika show hiyo kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka nchini Kenya, yenye lengo la kuleta burudani ya utofauti kwa wanamuziki wa Afrika, fashion pamoja na utamaduni.
Show hiyo inategemewa kufanyika (July 27) mwaka huu Nairobi, Kenya.

FILAMU MPYA YA AUNT EZEKIEL YAZUILIWA BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO



SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.


Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka  filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania.


“Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.

Kabla ya mwandishi wetu hajazungumza na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.
 

“Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa Aunt kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.


Alipotafutwa Aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.


Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada ya kuridhishwa na madai ya Kanisa Katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha Ukatoliki.

SHILOLE AMTIMUA MDOGO WAKE BAADA YA KUJAZWA MIMBA AKIWA MIKONONI MWAKE

STAA wa sinema za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtimua mdogo wake aliyekuwa akiishi naye aitwaye Mary baada ya kunasa ujauzito.
 

Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza habari kuwa, Shilole alifikia maamuzi hayo baada ya kumuonya binti huyo aachane na mwanaume aliyemjaza mimba hiyo lakini hakusikia hivyo akaona bora amtimue.
 
“Kamtimua baada ya kumuonya mara nyingi bila mafanikio akaona isiwe tabu bora aepuke aibu,” kilisema chanzo hicho.


Alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, mdogo huyo wa Shilole alikiri kutimuliwa na sasa amehamishia makazi kwa jamaa yake anayefahamika kwa jina la Tonny Montensi anayeishi Sinza, jijini Dar.

VIDEO YA WEMA SEPETU AKIWAPOROMOSHEA MATUSI MAZITO WAFANYAKAZI WAKE WA NDANI


STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi.  

Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.  

Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua tatizo. 

Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.

Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.

Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.  

Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na kuanza kutoa mkong’oto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele yake.

  Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni isiyoandikika  kutokana na ukali wake.

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD RAIS OBAMA


Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi.



Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.


Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.


Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.

Saturday, June 8, 2013

PHOTOS: Check Utengenezaji Wa Video Ya Vanessa Mdee “CLOSER” … Happy Birthday To Her …


1 Star2 Stars3 Stars4 Stars5 Stars


Msanii wa muziki Tanzania, Vanessa Mdee ambae pia alifanya vizuri sana kwenye ngoma na Ommy Dimpoz “Me n U” na mpaka kufikia kuingia katika nomination za Tuzo za KTMA na baadae kuachia ngoma yake ya CLOSER
Mpya kutoka kwa mwanadada huyu ni kuwa hivi sasa yuko mbioni kuachia video ya ngoma yake hiyo ya Closer … Video hiyo ambayo shooting yake imemalizika na leo mwanadada Vee anasheherekea siku yake ya kuzaliwa …
Kama sehemu ya kusheherekea siku yake hii, Vanessa ameamua kuachia baadhi ya picha za utengenezaji wa video hiyo …
Check picha hizo hapa chini …
closer....
closer.....
closer......
closer
closer.

SAKATA LA HOUSE GIRL ALIYEJINYONGA KISA PENZI LA CHRISTOPHER






Mfanyakazi wa ndani aliyejiua kisa mapenzi aitwaye Devotha Sanga leo ameagwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. 
Marehemu Devotha alijinyonga Juni 4 mwaka huu akiwa nyumbani kwa bosi wake eneo la Kitunda jijini Dar kwa wivu wa mapenzi. 
Devotha alikuwa katika penzi na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Christopher anayedaiwa kuwa na wapenzi wengi kiasi cha kusababisha marehemu kuchukua uamuzi huo. 
Baada ya kuagwa mwili wa Devotha umesafirishwa kuelekea Njombe kwa mazishi.

Friday, June 7, 2013

MWANAUME AFARIKI DUNIA NDANI YA URODA GEST HOUSE ILIYOKO MANZENSE LEO MCHANA......


Difenda  ya  polisi  ikiuchukua  mwili  wa  marehemu...

Mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina lake leo amekutwa amekufa katika gesti bubu iitwayo Uroda iliyopo Manzese Midizini jijini Dar. 


Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ni kwamba marehemu alikuwa na mpenzi wake ambaye waliingia wote katika gesti hiyo lakini alikutwa jamaa peke yake.

 Mwili wa marehemu umepelekwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL

WASHINDI WA TWEET ILIYOMKUNA REGINALD MENGI AKABIDHIWA KITITA CHA SH. MILIONI MOJA

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja mshindi wa kwanza wa shindano la,  "Tweet Wazo Jipya Kuondoa Umaskini", Jilly Gaudence Kyomo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dkt. Donath Olomi. 
Kulia ni mshindi wa pili, Peter George aliyejinyakulia shilingi laki tano na mwanafunzi wa chuo cha CBE, Ludovick Angelino, ambaye ni mshindi wa tatu aliyejinyakulia shilingi laki tatu

MAMBO 10 KUHUSU DIAMOND LIKIWEMO LA KUMILIKI ZAIDI YA BILIONI MOJA KATIKA ACCOUNT YAKE

1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.
3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.
4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.
6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.
7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.
8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.
9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.
10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk.

CHECK OUT WEMA SEPETU PAMOJA NA MIRAJI KIKWETE WAKIWA NA KUNDI LA MAKOLE HEXAGON KUTOKA DODOMA:

ERICK MSHANA KULIA KATIKATI WEMA SEPETU PAMOJA NA MIRAJI






 BAADHI YA KUNDI LA MAKOLE HEXAGONI KUIA NI SUDI NA MSABAHA KUTOKA MAKOLE KULIA NI ROMA & MIRAJI 
MAKOLE HEXAGONI NI KUNDI LINALOWAKILISHA DODOMA PANDE ZA MAKOLE AMBAPO WALIKUWEPO WAKIWAKILISHA MAKUNDI YOTE KUTOKA DODOMA MAKOLE HEXAGON PAMOJA NA EAST ZUU CAMP:WEBSITE HII INAPENDA KUTOA PONGEZI KUBWA SANA KUNDI LA MAKOLE HEXAGON AMBAO WAMEWAKILISHA VEMA KATIKA SAFARI YA MWISHO YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU  NGWEA, PONGEZI ZIKUFIKIE  ERICK MSHANA KUTOKA VODACOM ,SUDI BOY PAMOJA NA MSABAHA BILA KUMSAHAU BUSHOKE KWA USHIRIKIANO ALIOTOA AKIWA SOUTH NA WENGINE WENGI WALIOWAKILISHA MJI WA DODOMA:

MAREKANI YAUNDA SHERIA KUWADHIBITI WANAUME WANAOVAA SURUALI CHINI YA MAKALIO YAO

Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo ambao bado wako shuleni.
Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza mitaani.
Sheria hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
Unaonaje sheria kama hii ikija Tanzania pia?

HATIMAYE NGWEA AZIKWA KWENYE MAKABURI YA KIBONDA MKOANI MOROGORO....HIZI NDIO PICHA ZA MAZIKO YAKE

Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.

Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri.

 
 Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.
16f11344cea711e2813a22000a1f8f34_7
75e8603ecea511e29ecd22000aaa08de_7
4406673ccea511e2850422000a1f9a85_7
“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.


Naye Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpk hapa tulipomsindikiza panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”
e1147594cea211e2a86422000a1f9839_7
ee9d94facea411e2a9ea22000ae81462_7
f18745b2cea411e2aa3022000a9e2931_7

KHADIJA KOPA AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE JANA KWA AJILI YA MSIBA WA MUMEWE JAFFARI ALLY

Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki.
Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.

TASWIRA KUTOKA MSIBANI KWA MAMA MZAZI WA JAFFARI ALLY (MUME WA KHADIJA KOPA)

 Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu nyumbani kwake Tandale jijini Dar.

 Simanzi na majonzi vilitawala msiabani hapo.
Akina mama waliofika kumpa pole Mama Mzazi wa Jaffari.

SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, Tandale jijini Dar. 

Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana  katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

 Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake mzazi ni Mwenyekiti wa UWT Tandale.


 Mungu ailaze roho ya marehemu Jaffari Ally mahali pema peponi. AMEN!